Dira Yetu

Ni kuhakikisha kuwa maslahi ya wateja wetu yanalindwa kwa wakati, kupitia uelewa wetu thabiti wa mambo yahusuyo sheria na mazingira yanayotuzunguka.

Maono Yetu

Kuwa alama ya utoaji wa huduma, daima kuwa "hatua moja zaidi" ya wengine.

Sisi ni Nani

KAMPUNI YA SHERIA YA “LYSON LAW GROUP”

Lyson Law Group ni kampuni ya wanasheria wanaotoa huduma za sheria zenye ubora wa kimataifa na zenye kuzingatia asili ya Tanzania kwa umakini wa kina.

Kampuni ya sheria ya Lyson Law Group ilianzishwa mwaka 2019 na Bw.Victor Mwakimi na Bi. Lige James, mawakili wenye uzoefu na shauku ya kutoa huduma bora za kisheria kwa njia ya haraka na ya kuaminika, na wakati wote wakidumisha maadili muhimu ya uadilifu, uchapakazi na uaminifu; uaminifu kwa wateja wetu na kwa taaluma yetu nzuri.

Mwishoni mwa mwezi Februari 2021, Lawrence K. Masha Sr., Mshirika mkuu wa zamani wa makampuni mawili maarufu Dar es Salaam, ambaye alikua amestaafu sheria, akajiunga na Lyson Law Group kama Mwenyekiti wa Bodi na mshirika wa kudumu. Kujiunga kwa Bw. Masha kwenye Kampuni kunailetea Lyson Law Group uzoefu wa zaidi ya miaka 25 katika utendaji wa huduma za kisheria, katika maeneo yanayohusu shughuli za serikali na uongozi wa makampuni.

Lyson Law inashauri wateja wake kuepuka madai yasiyo ya lazima kwa kutumia mikakati ya kutokua na kesi, kulingana na kanuni kwamba "Kuzuia ni bora kuliko tiba". Hii imefikiwa kwa kuwasaidia wateja wetu kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa ndani kulingana na mtindo wa kipekee wa biashara ya kila mteja pamoja na utoaji wa maoni ya kisheria yaliyofanyiwa utafiti vizuri na kwa wakati ulio ombwa, hivyo kupunguza vipengele vya hatari ambavyo vinaweza kusababisha madai. Tuna amini kwamba madai daima huwa ni maamuzi ya mwisho. Hata hivyo, kwenye maswala ya ubishani, endapo upatanishi na usuluhishi vitashindikana, timu ya wanasheria ya Lyson Law Group daima itakuwa tayari kutetea maslahi ya Wateja wake kwa jitihada zote.

Timu ya Lyson Law Group, inajumuisha muunganiko mzuri wa ujuzi na uzoefu wa wataalam mbalimbali walioazimia kupiga hatua ya ziada ili kuhakikisha wanatoa suluhisho la uhakika kwa mahitaji ya wateja wetu na kufanya hivyo kwa namna ambayo ni “Hatua Moja Zaidi” ya wengine.