MAELEZO YA PROFAILI

    Lawrence K. Masha Sr.

  • Mwenyekiti / Patna
  • +255756444444 masha@lysonlaw.co.tz
  • Lawrence K. Masha, Mwenyekiti wa Bodi ya Lyson Law Group, alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania kuanzia mwaka 2008 hadi 2010. Mwenye shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Georgetown na shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Bw. Masha ana uzoefu wa zaidi ya miaka 25 kwenye uwanja wa sheria, utumishi wa umma na uongozi wa makampuni.

    Bw. Masha, ni mwanzilishi na Patna Msimamizi wa makampuni mawili ya sheria yanayoongoza Tanzania ambayo ni IMMMA Advocates (Mwanachama wa DLA Piper Africa) na Gabriel & Co, Attorney Law. Bw. Masha alichukua likizo ya miaka mitano kutoka katika uwakili wa kujitegemea alipochaguliwa kuwa Mbunge na hatimaye kujiunga na Baraza la Mawaziri la Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kama Naibu waziri wa Nishati na Madini na baadae kua Waziri wa Mambo ya Nje. Kabla ya kuanzishwa kwa IMMMA Advocates, Bw. Masha alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Oxygen Limited, Kampuni ya kwanza kuorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam.

    Bw. Masha kwa sasa anasimamia shughuli zote za ofisi zinazohusu masuala ya makampuni, benki na fedha, sheria za madini na mafuta, pamoja na sheria za uhamiaji, pia anashughulikia mahusiano ya serikali kwa niaba ya wateja wa kampuni

    Bw. Masha anaruhusiwa kufanya shughuli za kisheria pande zote mbili Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, na kwa mfulululizo alishika nafasi ya kua Mwanasheria mahiri kwa viwango vya vilivyowekwa na Law Chambers & Partners kabla hajaingia Serikalini kama mtumishi wa Umma.