MAELEZO YA PROFAILI

    Victor Mwakimi

  • Patna Msimamizi
  • +255752994870 vmwakimi@lysonlaw.co.tz
  • Bw. Mwakimi ni mwanzilishi na Patna Msimamizi wa kampuni ya sheria ya Lyson Law Group. Bw. Mwakimi ana uzoefu wa karibia miaka 10 kwenye uwanja wa sheria na amebobea katika sheria za makampuni, Benki na Fedha, Madai na sheria za Ardhi.

    Bw. Mwakimi alipata uzoefu na shauku ya uendeshaji wa mashitaka, kuandaa nyaraka za kisheria pamoja na ujuzi sheria za makampuni wakati akifanya kazi Trustworth Attorneys kama mkuu wa kitengo cha maswala ya  Ardhi na badae Gabriel & Co. Attorney at Law, ambapo alikuwa akisimamia huduma za makampuni, Benki na Fedha kama mkuu wa Kitengo.  Bw.Mwakimi alifanikiwa kufanya mambo mbalimbali ya kisheria ikiwemo maswala ya Ardhi, Mikopo ya Makampuni, Kodi za Makampuni na kuendesha kesi za madai ya Biashara.

    Bw. Mwakimi ni mwanasheria mzuri wa masuala ya sheria za makampuni na anajulikana kwa kazi zake kutokana na kujitolea kwake katika utoaji huduma na shauku ya utafiti katika eneo hili. Katika kipindi chote cha utendaji kazi wake, Bw. Mwakimi amefanikiwa kushughulikia changamoto na kazi mbalimbali za makampuni kwa niaba ya makampuni makubwa, benki na taasisi za fedha nchini Tanzania katika nyanja zote.

    Bw. Mwakimi ana shahada ya sheria na astashahada ya mafunzo ya sheria kwa vitendo pia ni mwanachama wa Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS).