MAELEZO YA PROFAILI

    Ms. Lige James

  • Patna Mtawala
  • +255755683316 ligejames@lysonlaw.co.tz
  • Bi. James ni wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania na mwanzilishi wa kampuni ya  sheria ya  Lyson Law Group, akiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika utendaji wa shughuli za kisheria. Bi. James, ni mwanasheria mwenye uzoefu katika sheria zinazohusu madai ya kampuni, na ubobezi katika nyanja zote za sheria ya ajira na mahusiano kazini pamoja na rasilimali watu. Bi.James mwenye shahada ya kwanza katika sheria na shahada ya uzamili katika Usimamizi wa Rasilimali Watu kutoka Chuo Kikuu cha Iringa (zamani kilikua Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini – Iringa).

    Bi. James anailetea kampuni mchanganyiko wa kipekee wa kuwa meneja rasilimali watu kwa miaka 5+ pamoja na kuwa wakili aliebobea katika sheria ya rasilimali watu. Kabla ya kuanzisha kampuni ya sheria ya Lyson Law, Bi. James alikuwa Msimamizi msaidizi wa kitengo cha sheria za ajira na mahusiano kazini katika kampuni ya sheria ya Gabrieli & Co. Bi. James amefanikiwa kuwawakilisha wateja wengi kwenye tume ya upatanishi na usuluhishi pamoja na Mahakama Kuu ya Tanzania - kitengo cha Kazi.  Mbali na sheria ya Rasilimali Watu, Bi. James ni mtaalamu wa Sheria ya Haki za Binadamu na sheria ya Uhamiaji